Mtoto wa Kiswidi anayedumisha mila ya Wamasai
Mtoto mwenye asili ya Uswidi (Sweden), Oscar Daudi ambaye mama yake ameolewa nchini Tanzania anapenda utamaduni wa kimasai na anajua kuongea kiswahili na kimasai.
Oscar mwenye umri wa miaka 11, anakaa Morogoro tangu akiwa na miaka saba.
Anatamani kuwa mfugaji na anajivunia utamaduni wa kimasai.
Yeye anavaa nguo za asili za kimasai peke yake.