Manusura wa mashambulio ya tindikali Uganda wazungumza
Unaposikia taarifa kuhusu watu kushambuliwa au kumwagiwa tindikali mwilini, mara nyingi ukatili huu huhusishwa na bara Asia. Hata hivyo kuna visa vingi vya watu kushambuliwa kwa tindikali ambavyo vinaripotiwa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki. Mwandishi wa BBC david Wafula amezungumza na baadhi ya manusuru wa mashambulio ya aina hiyo kutoka Uganda.