Idadi ya waandamanaji waliouawa Sudan yaongezeka hadi zaidi ya watu 100
Madaktari wanaohusishwa na vuguvugu la waandamanaji wanasema idadi ya watu waliouawa na vikosi vya usalama wiki hii imepanda na kufikia zaidi ya watu 100. Miili ya watu bado inaendelea kugundulika kufuatia harakati za kuwasambaratisha waandamanaji wanaotaka demokrasia nchini Sudan. Miili mingine zaidi imepatikana baada kuvutwa kutoka katika mto Nile nchini humo.