Visual Guide to the Women’s Africa Cup of Nations in Morocco (COPY) (COPY) (COPY)

Mwongozo wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake nchini Morocco

 

Hii itakuwa ni mara ya 15 kwa wanawake wa Afrika kumenyana katika kipute cha ubingwa wa bara hilo.

Lakini historia na muundo wa mashindano ya hapo awali bado haijanyooka. 

Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake 2024 (Wafcon) - ambazo ziliahirishwa hadi mwaka huu kwa sababu ya matatizo ya ratiba - zinashuhudia mataifa 12 yakichuana kuwania taji hilo nchini Morocco, ambapo mechi 26 zitachezwa katika viwanja sita vilivyopo katika miji mitano tofauti.

HISTORIA

Mashindano ya kwanza ya ubingwa wa Afrika kwa Wanawake yaliandaliwa mnamo 1991 ili kubaini mechi pekee ya bara hilo kufuzu kwa Kombe la Dunia la kwanza la Wanawake la Fifa. Timu nane zilitakiwa kushiriki kwa njia ya mtoano kwa kutumia mechi za nyumbani na ugenini, lakini mataifa manne yalijiondoa na Cameroon ilitinga fainali bila kucheza mchezo wowote.

Nigeria iliishinda Indomitable Lionesses jumla ya mabao 6-0 na kuwa mabingwa wa kwanza wa Afrika. Miaka minne baadaye, Super Falcons walishinda tena kwa kuishinda Afrika Kusini 11-2 kwa miguu miwili kwenye fainali.

Hata hivyo mashindano hayo mawili ya kwanza hayazingatiwi kuwa sehemu ya historia ya Wafcon (kwa hivyo haijajumuishwa katika takwimu ya nakala hii). Hilo linaanza mwaka wa 1998 wakati michuano hiyo ilipofanyika mara mbili ikijumuisha timu nane inayofanyika katika nchi moja mwenyeji, na hatua ya makundi kuanzishwa.

Nigeria iliandaa toleo la kwanza na kutawala - na hakuna mtu angeweza kuwaondoa Waafrika Magharibi mnamo 2000, 2002, 2004 na 2006 pia. Ni mwaka wa 2008 pekee ambapo Super Falcons hatimaye walivuliwa ufalme na mabingwa watetezi wa mwaka huo Equatorial Guinea.

Mwaka 2016 mashindano hayo yalibadilishwa jina kuwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake, na kuifanya iwiane na mashindano sawia na hayo upande wa wanaume.

Toleo la 2020 halikufanyika kufuatia janga la coronavirus. Wakati Wafcon iliyopanuliwa iliporejea mwaka wa 2022, ambayo sasa inajumuisha timu 12. Afrika Kusini waliwashinda wenyeji Morocco na kufuta maumivu ya kushindwa mara nne katika fainali.

 

 

WASHINDI NA REKODI

Ni mataifa matatu pekee ambayo yamewahi kushinda Wafcon. Nigeria watakuwa wanawania taji la 10 nchini Morocco, huku Equatorial Guinea wakishinda kombe hilo mara mbili (mara zote wakiwa wenyeji) na Afrika Kusini mara moja.

Cameroon, Ghana na Morocco ndizo timu nyingine zilizotinga fainali.

Afrika Kusini wamemaliza wa pili mara nne, huku Cameroon na Ghana zikiwa zimepoteza fainali tatu kila moja.

Akiwa na mabao 34, Perpetua Nkwocha wa Nigeria ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Wafcon. Mshindi mara nne wa kiatu cha dhahabu, mabao yake 11 mwaka 2010 yanasalia kuwa rekodi ya mashindano moja.

WENYEJI WA MICHUANO

Mashindano ya 2020 yalifutwa kwa sababu ya janga la Covid-19.

VIWANJA NA MECHI ITAKAPOCHEZWA

MUUNDO

Katika hatua ya makundi, timu 12 zimepangwa katika makundi matatu ya nne.

Timu mbili za kwaza zitatinga robo fainali pamoja na timu mbili bora zilizoshika nafasi ya tatu.

WACHEZAJI WA KUTAZAMWA

Asisat Oshoala (Nigeria)

Sasa anaichezea Bay FC katika Ligi ya Kitaifa ya Soka ya Wanawake ya Marekani (NWSL), mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 analeta tajiriba ya uzoefu na mawazo ya kushinda katika fainali ambazo zitakuwa za sita za Wafcon.

Mwanasoka huyo bora wa mwaka wa kike wa Kiafrika mara sita alisaidia Super Falcons kuchukua taji la bara mnamo 2014, 2016 na 2018, na tangu wakati huo pia ameshinda Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mara mbili akiwa na Barcelona.

Ingawa hakuwa na uwezo mkubwa mbele ya lango tangu ahamie Marekani, Oshoala bado ana muonekano wa nyota na huenda akawa kiungo muhimu atakayeamua ikiwa Nigeria inaweza kushinda tena taji la Wafcon.

Clara Luvanga (Tanzania)

Luvanga ana malengo makubwa, baada ya kuiambia BBC kwamba anataka kuwa mchezaji bora zaidi barani Afrika, na tayari ameshinda mataji mawili nchini Saudi Arabia akiwa na Al-Nassr.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana fursa ya kujifunza kutoka kwa walio bora zaidi, huku Cristiano Ronaldo na Sadio Mane wakiwa kwenye orodha ya upande wa wanaume wa klabu yake. Luvanga alifunga mabao 19 ya ligi msimu uliopita, na hivyo kumfanya kuwa wa nne kwenye chati za Ligi ya Saudia.

Kufunga mabao katika mechi zote nne za maandalizi ya Wafcon ya Tanzania kunathibitisha kwamba ni moto wa kuotea mbali ukizingatia kasi na nguvu yake. Mabeki watajua uwezo wake, lakini je, wanaweza kumzuia?

Sanaa Mssoudy (Morocco)

Kiwango cha fowadi huyo mwaka wa 2024 kilimfanya kutajwa kuwa mchezaji wa thamani zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ya Wanawake na kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa vilabu barani Afrika.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 pia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Morocco msimu uliopita, aliisaidia AS FAR kushinda taji la 12 la nyumbani.

Mssoudy alifunga katika robo- na nusu fainali ya Wafcon iliyopita. Je umahiri wake unaweza kuisaidia Wanasimba wa Atlas kumaliza udhia wa taji kuu la bara? 

Jermaine Seoposenwe (South Africa)

Afrika Kusini itamtegemea Seoposenwe mwenye uzoefu mkubwa kwa mabao hasa baada ya Thembi Kgatlana, mshindi wa kiatu cha dhahabu katika WAFCON 2018, kujiondoa kwenye kikosi kwa sababu binafsi.

Kama ilivyo kwa Kgatlana, Seoposenwe, mzaliwa wa Cape Town, sasa anacheza soka lake nchini Mexico. Mshambuliaji huyo wa Monterrey mwenye umri wa miaka 31 atakuwa mmoja wa wachezaji wakongwe wa Banyana Banyana, akiwa amecheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Zimbabwe mnamo mwaka 2010.

Akiwa ameichezea timu yake zaidi ya mechi 100, Seoposenwe ametangaza kuwa atastaafu soka la kimataifa baada ya WAFCON. Atalazimika kufunga mabao awezavyo katika fainali zake za sita ikiwa Afrika Kusini inatumai kutetea taji lake. 

Aissata Traore (Mali)

Alifunga mabao manne katika mechi za kufuzu huku wachezaji wa Afrika Magharibi wakipiku kirahisi Jamhuri ya Afrika ya Kati na Guinea na kurejea kwenye fainali hizi kwa mara ya kwanza tangu 2018.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa mfungaji bora akiwa na Fleury katika Ligi Kuu ya Ufaransa msimu wa 2024-25, akiwa na mabao tisa, huku klabu hiyo ikimaliza nje kidogo ya nafasi za kufuzu Ulaya.

Akiwa sehemu ya kikosi cha Mali kilichomaliza nafasi ya nne katika kushiriki kwao WAFCON ya hivi karibuni, Traore anatengeneza safi kali ushambuliaji pamoja na Agueicha Diarra wa Paris St-Germain. Wote wawili watatumai kurudia kiwango kikubwa cha ufungaji mabao walichofurahia katika mechi za kufuzu.

Barbra Banda (Zambia)

Kwa kifupi, Banda ni mashine ya mabao.

Akiwa na mabao 10 katika michezo ya Tokyo na Paris, yeye ndiye mfungaji bora wa muda wote barani Afrika, katika mashindano ya Olimpiki, huku mchezaji bora wa soka la wanawake wa mwaka wa BBC wa sasa akimaliza wa pili katika msimamo wa NWSL msimu uliopita, akifunga bao muhimu na kuipa Orlando Pride ushindi wa 1-0 katika fainali.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 bado hajafunga bao lolote kwenye WAFCON, akiwa amekosa fainali za 2022. Akiwa wa pili kwenye orodha ya wachezaji wa kike ghali zaidi barani Afrika, Banda atakuwa na hamu ya kurekebisha hilo nchini Morocco.

MABAO KATIKA KILA SHINDANO

ZAWADI

Mara ya mwisho, zawadi ya pesa taslimu ya Wafcon ziliongezeka zaidi ya mara mbili, na kuongezeka kutoka $975,000 (£720,000) mwaka wa 2018 hadi $2.4m (£1.8m) mwaka wa 2022. Washindi Afrika Kusini walipokea $500,000 (£370,000).

WALIOFUATILIA

Zaidi ya mashabiki 50,000 walitazama fainali ya 2022 kati ya Morocco na Afrika Kusini kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat - rekodi ya mechi ya Wafcon.

NANI ATASHINDA

Barabara zote zitaelekea kwenye Uwanja wa Olimpiki huko Rabat kwa fainali siku ya Jumamosi, 26 Julai.

Uwanja huu mpya chenye uwezo wa kuketi watu 21,000 kimejengwa kama sehemu ya uendelezaji mpana wa eneo la kihistoria la Uwanja wa Prince Moulay Abdellah. Uwanja huo mkubwa, uliokuwa mwenyeji wa fainali za WAFCON 2022, unajengwa upya kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 na Kombe la Dunia 2030.

Morocco imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye soka, Je timu ya wanawake ya nchi hiyo inaweza kufanua maajabu? na kubeba taji lake la kwanza la WAFCON? Nigeria, Zambia, na mabingwa watetezi Afrika Kusini ni timu nyingine zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo.

Credits 

Imeandikwa na Ian Williams na Rob Stevens
Imebuniwa na Thiago Braz
Utafiti wa ziada umefanywa na Eshlin Vedan
Picha: Getty Images na BackPage Pix