Episode details

BBC,2 mins
Mkasa wa binti kubakwa Tanzania, uchunguzi umefikia hatua nzuri- Msemaji wa polisi
Available for over a year
Jeshi la polisi nchini Tanzania limesema uchunguzi kuhusu mkasa wa kubakwa kwa binti mtanzania ulifanywa na kundi la wanaume watano umefikia pazuri na kuwataka wananchi kuwa na subira. Muda mfupi uliopita Mwandishi wa BBC, Martha Saranga amezungumza na Msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania David Misime na kwanza amemuuliza uchunguzi umefikia hatu agani? Hata hivyo taasisi mbalimbali zimekemea tukio hilo ikiwemo chama cha mawakili tanzania TLS, na tume ya kutetea haki za binadamu wakitaka sheria kali zichukuliwe. Nae waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa nchini Tanzania Dr Stagomena Tax amenukuliwa na chombo cha habari nchini Tanzania akisema Serikali haitavumilia uvunjaji wa sheria,na atakayebainika kutekeleza ukatili huo atachukuliwa hatua stahiki. Mwishoni wa wiki iliyopita, video ikimuonesha binti akifanyiwa vitendo vya ukatili na kundi la vijana watano ilisambaa nchini Tanzania na kuzua gumzo na hasira miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Programme Website